03 Jun 2023 / 128 views
Phil Neville afukuzwa ukocha Inter Milan

Klabu ya Inter Miami ya Marekani imemfuta kazi kocha wake Phil Neville kutokana na matokeo mabovu wanayopata klabu hiyo kwenye ligi ya Marekani.

Juzi timu hiyo ilipoteza 1-0 dhidi ya New York Red Bulls wakiwa nyumbani ambapo ilikuwa mechi ya 10 kupoteza akiwa amecheza mechi 13 kwenye ligi.

Neville mwenye umri wa miaka 46 alichaguliwa kuwa kocha wa klabu hiyo Januari 2021 na kufanikisha timu hiyo kucheza mechi ya mtoano wa kombe la Marekani mwaka 2022.

"Wakati mwingine katika mchezo huu tunapaswa kufanya maamuzi magumu zaidi," alisema mmiliki mwenza wa klabu hiyo David Beckham.

"Cha kusikitisha tunaona wakati ni sahihi kufanya mabadiliko. Nataka binafsi kumshukuru Phil kwa bidii yake, mapenzi yake kwa klabu yetu na kwa uadilifu wake kama mtu."

Mchezaji mwenzake wa zamani wa Manchester United na England na Neville, Beckham aliongeza: "Yeye na familia yake walikumbatiana na Miami na amejitolea katika harakati za kuleta mafanikio katika jiji hilo na kwa mashabiki wetu.

"Phil ametoa mchango wa kweli kwa utamaduni wa klabu yetu na sifa zake kama kiongozi na ujuzi kama kocha."

Neville alikuwa kocha wa timu ya wanawake ya Uingereza kwa miaka mitatu alipoacha jukumu hilo na kuchukua kazi Miami.

Kocha Msaidizi Jason Kreis pia ameondoka Inter Miami, huku msaidizi mwenzake Javier Morales akichukua nafasi hiyo kama kocha mkuu wa muda kabla ya mchezo wa nyumbani wa Jumamosi dhidi ya DC United.